Habari

Video: Serikali yaweka mikakati hii kupunguza ajali za bodaboda

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema serikali itatoa elimu ya usalama barabarani mashuleni na kupitia vituo vya redio ili kupunguza ajali za bodaboda nchini.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kaliua (CUF),Magdalena Sakaya lililohoji

Kwa kuwa lengo la serikali kuruhusu vyombo vya usafiri wa pikipiki kubeba abiria na mizigo, ni kusaidia kurahisisha usafiri na pia kutoa ajira hapa nchini, lakini ajali ni nyingi kuliko vyombo vingine, Je serikali ina mikakati gani ya uhakika ya kuokoa maisha ya nguvu kazi ya taifa inayopotea kwa usafiri huo?

“Katika miaka mitatu toka Januari 2015 hadi Februali 2017 jumla ya ajali 5,518 za bodaboda zilitokea na kusababisha vifo 1,945 na majeruhi 4,696. Serikali kupitia Jeshi la Polisi inayo mikakati ya kuokoa maisha na nguvu kazi inayotakana na ajali hizi za bodaboda,” alisema Mwigulu Nchemba.

“Mikakati hiyo ni pamoja na kupitishwa kwa kanuni ya leseni ya pikipiki na bajaji iliyopita mwaka 2009, pili kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni na kupitia vituo vya redio pamoja vipeperushi. Tatu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa waendesha bodaboda, nne kuimarisha usimamizi wa usalama barabarani, tano kusisitiza madereva bodaboda kuepuka kuendesha kwa mwendokasi hatua ya sita kuchukua hatua kwa vitendo vyote vya ulevi na kusisitiza matumizi ya kofia ngumu ili kupunga madhara pindi ajali zinapojitokeza.” aliongeza.

Video: Tazama majibu ya Serikali,


Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents