Habari

Video: Wadau wa Takwimu watakiwa kufuata sheria – NBS

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imwataka wadau wa Takwimu Nchini kufuata kanuni na taratibu za utoaji takwimu ili kuepusha sintofahamu baina yao na wapokeaji taarifa na Taasisi husika.

Akizungumza na Wanahabari, Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa leo kufuatia taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Kampuni ya Utafiti ya Geopoll yenye ofisi ya Kanda ya Afrika, mjini Nairobi, Kenya kuhusiana Viwango na Idadi ya watazamaji wa vituo mbali mbali vya habari vinavyorushwa hapa nchini

“Taarifa zozote zinazohusu utafiti ni lazima zihusishe wadau mbalimbali na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa na mamlaka iliyoidhinishwa kisheria kuhusiana na utoaji takwimu”, Dkt.Chuwa ambapo alisema vigezo hivyo ni uwazi na ukweli, uhusishwaji wa Wadau na kwa kuzingatia weledi.

Video:

Na Emmy Mwaipopo & Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents