Burudani

Video ya ‘Nagharamia’ ya Christian Bella ilikuwa iongozwe na Clarence Peters wa Nigeria

Christian Bella amesema alipanga kufanya video ya wimbo wake ‘Nagharamia’ na muongozaji wa nchini Nigeria, Clarence Peters lakini ilishindikana kutokana na muda na hivyo kuamua kufanya na Enos Olik wa Kenya.

Bella na Ali Kiba

Bella ambaye alisafiri hivi karibuni na Alikiba kwenda nchini Afrika Kusini na kufanikisha ku-shoot video hiyo, ameimbia Bongo5 kuwa kama Clarence Peters angefanya video hiyo, asingeweza kuutoa mwaka huu.

“Mwisho wa siku sisi tunawasikiliza mashabiki wa muziki wetu. Clarence Peters alikuwa yupo tayari kufanya kazi lakini isingetoka kwa wakati, sasa sisi hatukutaka iwe hivyo,” amesema.

“Mashabiki walihitaji kazi kwa haraka basi tukaamua kumchukua Enos Olik na sasa hivi navyokwambia wiki ijayo ngoma na video inaweza kutoka,” ameongeza.

Clarence ndiye aliyeongoza video ya Number One Remix ya Diamond aliyomshirikisha Davido.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents