Fahamu

Vita vya pamba moto Azerbaijani na Armenian 

Vikosi vya jeshi la Azerbaijani na Armenian vimekataa wito wa kumaliza mzozo katika eneo la kusini mwa Caucasus, eneo ambalo mapigano yameongezeka hivi karibuni.

Alhamisi, Urusi na Ufaransa zimetaka kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea ukanda wa Nagorno-Karabakh, eneo ambalo lina ghasia kubwa ambazo hazijawahi kutokea kwa miongo.

Lakini makombora na milipuko mikubwa imeripotiwa katika mji mkuu nyakati za usiku.

Upande wa mamlaka ya Azerbaijan, eneo ambalo linaongozwa na jamii ya Armenians.

Jamuhuri mbili za zamani za ‘Soviet’ zilipigana vita mwaka 1988-94 dhidi ya himaya yao.

Ingawa Armenia ilitangaza kuwa hailitambui taifa hilo rasmi.

Haijawa wazi chanzo cha mapigano hayo kurejea, yalianza Jumapili na ni makubwa kutokea tangu mapigano ya mwaka 1994 .

Watu kadhaa wameuawa na mamia kujeruhiwa , na kukiwa na hofu kuwa nguvu za kimataifa zitaingilia mgogoro huo.

Nini kinaendelea sasa?

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Urusi Vladimir wamejadili kuhusu uhitaji wa haraka wa kupunguza ghasia katika eneo hilo.

“Wamekubaliana kuhusu uhitaji wa kushirikiana kwa pamoja ili kukabiliana na mapigano hayo,” taarifa kutoka ofisi ya rais Macron ilieleza kupitia njia ya simu.

“Tunataka pande zote mbili zisitishe mapigano haraka iwezekanavyo, kwa kuwa mvutano huo unasababisha eneo hilo kuekewa kizuizi cha hali ya juu,” taarifa kutoka Kremlin zilisema.

Urusi ilitaka kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Armenia pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Azerbaijan.

Urusi ni sehemu ya jeshi la Armenia na ina kambi ya jeshi nchini humo. Hata hivyo ina uhusiano mzuri na serikali ya Azerbaijan.

Baada ya bwana Macron na bwana Putin kufanya mazungumzo, Kremlin ilitoa tamko kuwa wamejadili jinsi ya kusonga mbele kwa shirika la usalama wa Minsk Group ambalo lina ushirikiano na ulaya (OSCE) ili kusaidia kutatua mgogoro huu.Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Urusi Vladimir wamejadili kuhusu uhitaji wa haraka wa kupunguza ghasia katika eneo hilo.

Kundi la Minsk lilianzishwa mwaka 1992 na kuongozwa na Ufaransa , Urusi na Marekani.

Viongozi wote walionyesha utayari kuona taarifa hiyo kwa niaba ya kundi lao ambalo limetaka kusitishwa kwa mapigano hayo na kutaka mazungumzo ya amani kufanyika.

Mapigano yaliyoanza Jumapili yamesababisha vifo vya wanajeshi na raia pia.

Ofisi ya bwana Macron imeelezea wasiwasi wake kuhusu ripoti ya wanajeshi wa Syrian kusafirishwa mpaka Azerbaijan kwa kutumia kampuni ya kijeshi ya uturuki.

Mpiganaji mmoja aliiambia BBC Arabic, mapema wiki hii kuwa alikuwa amepewa ajira kaskazini mwa Syria na kupelekwa Uturuki kwa ajili ya kupigana katika mgogoro huo.

Abdullah – si jina lake halisi -alisema alitumwa Nagorno-Karabakh “kuvaa sare za kijeshi za Azerbaijani” mara tu vita ilipoanza.

Lakini Uturuki ilikanusha madai hayo na mshauri wa rais wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan alipinga ripoti hiyo kuwa si ya kweli kabisa na haipo.

Balozi wa Azerbaijan, nchini Marekani pia amekanusha taarifa hiyo ya kuhusishwa Uturuki.

Muangalizi wa Syria wa ripoti ya haki za binadamu inayosema wanajeshi wapatao 900 walisafirishwa mpaka Azerbaijan na kampuni ya Uturuki .

Lakini waliongeza kuwa wapiganaji wa Armenian-walizaliwa nchini Syria pia wamesafirishwa mpaka Armenia ili kupigana.

Hatari ya vita kuongezeka katika ukanda huo

Uchambuzi wa Laurence Broers, Kutoka kusini mwa Caucasus

Ongezeko la awali la vikosi vya jeshi kati ya Armenian na Azerbaijani baada ya siku chache. Kutuliza ghasia zinazoendelea linaweza kuwa jambo lisilowezekana kwa sasa.

Maeneo ya watu wengi ndani ya himaya ya Nagorno-Karabakh yamepigwa na makombora mengi na mabomu, hali ambayo haijawahi kutokea tangu mwaka 1990.

Raia wakiwa wanalengwa Armenia na hata wananchi wa Azerbaijan wamekuwa wakipigwa pia.

Pande zote mbili zinaonekana kutaka ghasia kuwa za muda mrefu.

Azerbaijan imekataa kufanya makubaliano na Armenia, na ukilinganisha na mgogoro wa awali vita ya sasa inaonekana kuwa kubwa kwa kuwa wanaungwa mkono na Uturuki.

Hatari ipo kwa muda mrefu, mgogoro ukiwa unaonekana kuongezeka na unaweza kuhusisha nguvu za mataifa ya kigeni.

Nini kinachoendelea katika vita?

Makombora makubwa yanaendelea mpaka leo, na kila upande ukidai kuwa uharibifu mkubwa umetokea.

Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan ilisema ilifanya mapigano dhidi ya jeshi la Armenian usiku wote.

Hata hivyo , maofisa wa Nagorno-Karabakh walisema hali ni mbaya na kumekuwa na majibishano ya risasi.

“Adui alijaribu kuwavamia lakini wanajeshi wa Armenian walikabiliana na jaribio hilo” taarifa ilielezwa , kwa mujibu wakala wa habari AFP.Waandishi wawili wa Ufaransa wa gazeti la Le Monde wamejeruhiwa karibu na mji wa Armenian, Martuni.

Waandishi wawili wa Ufaransa wa gazeti la Le Monde wamejeruhiwa karibu na mji wa Armenian, Martuni.

Azerbaijan ilichapisha video inayosema uharibifu wa maadui wawili katika kijiji cha Tonashen.

Vyombo vya habari vya Armenian vimesema raia watatu wameuawa huko Azerbaijani katika shambulio la anga katika eneo la soko siku ya Jumatano.

Chombo cha habari cha taifa la Armenpress kimesema wananchi saba na wanajeshi 80 waliuliwa wakati mapigano yalipoanza.

Wizara ya ulinzi ya Armenia pia ilitoa taarifa ya picha ya ndege ya Armenian SU-25 ikiwa imetunguliwa Jumanne na ndege ya Uturuki Turkish F-16. Huku Uturuki ikikanusha madai hayo na kudai kuwa ni propaganda zisizo na maana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents