Vurugu zote Simba ilikuwa ni mdomo wa Haji Manara, watafanya vibaya – Dr Sule

Mhadhiri na mhutubu maarufu Dr Sule amedai kuwa maneno ya aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Simba SC Haji Manara yalikuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo na wala sio kuwa watani wao wa jadi Yanga walikuwa hawana timu lahasha.

Dr Sule anaamini Simba msimu ujao haitakuwa na mafanikio makubwa ukilinganisha na miaka hiyo minne ambayo Manara alikuwa akiitumikia kwakuwa anaamini ‘Propaganda’ za Marana zilikuwa na nguvu na kuwaogopesha wapinzani.

”Vurugu zote mlizoziona miaka minne za Simba ni mineno ya Manara basi, sio kwamba Yanga walikuwa hawana timu lakini ule mdomo wa Manara ulikuwa unawatisha, mkitaka kubisha subirini baada ya kutoka kwake mtaona kama itafanya vizuri mwakani Propaganda ni kitu kikubwa kuliko mnavyofikiria.”- Dr Sule

Kuangalia video bofya HAPA

Related Articles

Back to top button