Habari

Vyombo vya dola viwasake waliohusika tukio la Mhe. Lissu – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio la kinyama la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu lililotokea mchana wa Alhamisi hii mjini Dodoma.

Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, kwa kuandika amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo.

“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” ametweet Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents