Habari

Wabunge wafanya ziara Ofisi za OSHA na viwandani (+Video)

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wamefanya ziara katika ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili kujionea jinsi Taasisi hiyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inavyosimamia uzingatiaji wa viwango vya usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini.

Ziara hiyo imetokana na taarifa ya utekelezaji majukumu ya OSHA kwa mwaka 2020/2021 iliyowasilishwa kwenye Kamati hiyo mwezi Machi ambapo Kamati iliridhishwa na utendaji na hivyo kuagiza kuandaliwa kwa ziara kwa ajili ya Kamati kupata uhalisia wa masuala ambayo wamekuwa wakiwasilishiwa kupitia taarifa mbali mbali.

Baada ya kutembelea ofisi za OSHA, kiwanda cha Sigara TCC na kiwanda cha Gypsum cha Knauf kilichopo Mkuranga ambako walikwenda kutazama jinsi viwanda hivyo vinavyotekeleza miongozo inayotolewa na OSHA, Kaimu Mwenyekiti na Wajumbe
wa Kamati hiyo, wamesema wameridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na OSHA katika kutoa miongozo ya kulinda nguvu kazi katika maeneo ya kazi hapa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema serikali imekuwa ikitegemea sana ushauri wa Kamati za Bunge ili kuweza kutekeleza mipango yake ipasavyo.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema kupitia ziara hiyo wajumbe wa Kamati wamepata fursa ya kujionea hali halisi ya usalama na afya katika maeneo ya kazi hapa nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents