Waingereza washerehekea kuondolewa kwa masharti ya Corona (+ Video)

Siku ya jana Serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa imeamua kuondoa masharti yote ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona (Lockdown) na kuwataka Wananchi kuendelea kuwa waangalifu huku wakiendelea na shughuli zao za kawaida cha msingi kila mmoja achukue hatua binafsi.

Mbali na masharti hayo kuondolewa tabu ilikuwa kwenye vilabu vya starehe navyo vyote kuanzia jana vinaruhusiwa kufunguliwa na pia, kuvaa Barakoa, kukaa umbali wa mita moja na nusu baina ya Watu na kufanya kazi kutoka nyumbani vyote vimefutwa.

Ikumbukwe taifa la Uingereza ni moja ya mataifa ambayo yalitangaza kulichukulia janga na Corona kama magonjwa mengine na walieleza kuwa wataishi nalo kama wanavyoishi na magonjwa mengine cha msingi ni kila mmoja kuwa muangalifu na kuchukua tahadhari binafsi.

Kwenye mpira pia mashabiki wanatarajiwa kurudi viwanjani kwani ligi kuu Uingereza inatarajiwa kuanza mnamo tarehe 14/8/2021 hivyo mashabiki wataruhusiwa kuingia viwanjani kama kawaida ila barakoa na tahadhari nyingine ni muhimu kuchukuliwa.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye vilabu vya starehe usiku wa jana.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/tv/CRituuXDdZq/

Related Articles

Back to top button