Burudani

Wakali Kwanza kurejea na ‘Siishiwi Hamu’

Wakali Kwanza, kundi lililowahi kutikisa mawimbi ya redio na TV nchini kwa nyimbo kama Natamani na zingine, linatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia kazi mpya iitwayo ‘Siishiwi Hamu.’

14156523_168978550173841_59092201_n

Q-Jay ambaye ni mmoja wa members watatu wa kundi hilo wakiwemo Makamua na Joslin, alikiambia kipindi cha Mdundo Bado cha Lake FM kuwa kundi lao bado lipo pamoja na imara.

Q amesema baada ya kuachia mradi wa pamoja wa Wakali Kwanza ataachia pia kazi yake kama solo. Amedai kuwa Siishiwi Hamu itatoka pamoja na video yake na ni wimbo uliofanyika MJ Records.

Ukimya wake Q Jay amedai kuwa ulitokana na kuamua kumrudia mwenyezi Mungu lakini kutokana na kuupenda muziki ameamua kuendelea na muziki wa kawaida lakini wenye mafundisho zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents