Siasa

Waliotengeneza habari 2009

Image
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Utawala wake mwaka huu umekuwa kwenye macho ya wengi hasa kwenye vita dhidi ya ufisadi na umaskini. Amekuwa akipingwa na badhi ya wazee wa CCM. Ujihusishaji wake kwenye jamii umedhihirika kwa hali ya juu

Image
RAIS BARACK OBAMA
Tuzo yake ya Nobel imeibua mjadala mkubwa duniani. Alianza kutengeneza habari baada ya kujitosa kugombea urais wa Marekani na kuchukua mwanzoni mwaka huu.Harakati zake za kuleta udiplomasia wa kimataifa zimeboresha mahusiano kati ya Marekani na nchi nyingine


HASHIM THABEET
Mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu Marekani. Hashim (futi 7’3) alichaguliwa kucheza ligi hiyo kubwa zaidi ulimwenguni katikati ya mwaka na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa. Mapumziko yake mafupi nchini yalivuta ya vyombo vya habari


STEVEN KANUMBA
Stori za jamaa huyu kuchemka kimombo wakati akiwa kwenye jumba la Big Brother zilisikika na kuonekana sana kwenye vyombo vya habari ingawa mwenyewe alijitokeza na kupinga madai hayo.Filamu zake bado zimeendelea kutamba na kumfanya awe juu maradufu


ELIZABETH GUPTA
Mshiriki wa pili wa kike kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Big brother africa. Elizabeth alijitahidi sana kupambana na ingawa hakufanikiwa kupata ushindi, aliacha picha nzuri na wenzake walimheshimu
TIGER WOODS
Ukiwembe wa mcheza gofu huyu ulivuta vyombo vya habari na kutishia heshima yake kwenye mchezo huo, hasa baada ya vimwana 11 kujitokeza na kudai kula uroda na jamaa na mke wake kuangalia uwezekano wa talaka
MICHAEL JACKSON
Yote yalianza baada ya kutangaza kufanya shoo 50 huko London na baadaye kifo chake baada ya kuzidiwa na madawa. Kifo cha Michael nusura kiharibu mtandao baada ya mabilioni ya washabiki zake kutumiana meseji za habari hiyo. Michael aliliwa na dunia nzima
WEMA SEPETU
Wema ameuza mamilioni ya magazeti ya udaku kwa skendo zake ukianzia kwa vurugu na mpenzi wake wa zanami, Steven kanumba, kulala selo na mpaka ujauzito wake wa sasa
UMAGA
Eddie Eki Fatu aka Umaga alifariki wiki chache zilizopita kwa maradhi ya moyo na kuacha simanzi kwa wapenzi wa mieleka. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
FIESTA ONE LOVE
Hamna ubishi hili ndilo tamasha lililovuta wengi mwaka huu hasa baada ya kumleta mkali wa kufoka kutoka Marekani, Busta Rhymes ambaye aliangusha shoo ya ukweli akiwa na mwana wake wa Flipmode, Spliff Star

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents