Burudani

Wasanii watatu wa label ya The Industry wapo tayari kuingia vitani

Mkurugenzi wa label ya The Industry, Nahreel amefunguka kwa kusema kuwa maandalizi ya kuwaleta wasanii wa label hiyo yapo katika hatua za mwisho.
aaa
Mmoja kati ya wasanii wa label ya The Industry, Rose

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nahreel amesema tayari wasanii hao watatu kila mmoja ana video yake mkononi ambayo imeandaliwa Afrika Kusini na director Justin Campos.

“Hivi sasa kila msanii anakaribia kukamilisha albamu yake, na tuna video ambazo zipo tayari za wasanii wote watatu na video zimeandaliwa Afrika Kusini na Justin Campos, kwa hiyo sasa hivi tunaangalia jinsi ya kuanza kurelease moja baada ya nyingine,” alisema Nahreel.

Kwa upande wa Kundi la Navy Kenzo, Nahreel amesema wanajipanga kuja kivingine huku akiweka wazi ujio wa kobalo yao na mkali wa Aje, AliKiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents