Burudani

Watu wawili wauawa kwa risasi kwenye show ya Meek Mill

Polisi wamedai kuwa watu wawili wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa nje ya ukumbi huko Connecticut Ijumaa iliyopita baada ya Meek Mill kumaliza kutumbuiza.

Msemaji wa polisi wa Wallingford alidai kuwa maofisa walifuatilia ripoti za kupigwa kwa risasi hizo nje ya ukumbi wa Oakdale Theatre. Maofisa waliwakuta watu wawili wakiwa wamekufa.

Polisi bado hawajatangaza majina ya waliopoteza maisha na kwamba mtu mmoja anashikiliwa. Hakuna uhusiano kati ya show ya Meek Mill na mauaji hayo hadi sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents