Technology

Watumiaji wa WhatsApp wasiofuata masharti mapya kukosa huduma ifikapo tarehe hii

Watumiaji wa mtandao wa WhatsApp ambao hawatafuata masharti mapya na vigezo mpaka kufikia tarehe 15 mwezi Mei hawataweza kupokea au kutuma ujumbe mpaka wakubali masharti hayo.

Akaunti zao zitaorodheshwa kama ”zisizofanya kazi”. Na akaunti zisizofanya kazi zinaweza kufutwa baada ya siku 120.

Simu na ujumbe wa arifa utafanya kazi kwa ”muda mfupi” lakini TechCrunch imeripoti, labda kwa ”wiki chache”.

WhatsApp ilitangaza mabadiliko mwezi Januari.

Kulikuwa na mapingamizi miongoni mwa watumiaji ambao walidhani ilimaanisha kuwa kampuni ilikuwa ikipanga kubadili kiasi cha data inazotoa kwa kampuni mama, Facebook.

Baadaye ilifafanua hii haikuwa hivyo – isipokuwa inalenga kuwezesha malipo kufanywa kwa wafanyabiashara.

Kuwajulisha watumiaji

WhatsApp tayari inatoa taarifa ikishirikisha taarifa kwa Facebook, kama vile anuani ya IP (nambari zinazoambatanishwa kwenye kila kifaa kinachojiunga na intaneti, inaweza pia kutumika ili kufahamu mahali kifaa hicho kilipo) na kufanya manunuzi kutumia jukwaa hilo.

Lakini hali haiku hivyo Ulaya, ambako kuna sheria za faragha.

Kufuatia tangazo la awali, majukwaa kama Telegram na Signal yalishuhudia kuongezeka kwa mahitaji, watumiaji wa WhatsApp wakitafuta huduma mbadala za kutuma ujumbe.

WhatsApp ilichelewesha uchapishaji wa awali na sasa imebadilisha jinsi inavyowarifu watumiaji mabadiliko hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents