HabariSiasa

Waziri apiga marufuku Wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amepiga marufuku Wanafunzi kucheza nyimbo zisizo na maadili na kuwataka Walimu kuwa wasimamizi wa tabia za Wanafunzi wawapo shuleni.

Mkenda amesema hayo nje ya Bunge jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu picha ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha Wanafunzi wakicheza wimbo wa Zuchu ‘Honey’.

“Tumeshatambua shule yenyewe iko Tunduma, kulikuwa na kikundi kimeenda kutoa msaada shuleni pale, baada ya kutoa msaada ule kikaweka na muziki halafu Wanafunzi wakacheza na maudhui ya muziki wenyewe kila mtu ameusikia sina haja ya kuurudia”. amesema Profesa Mkenda

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wa watoto kusimamia malezi kwani ni jukumu la kila mmoja.

“Napenda kuchati na jamii kwenye Instagram nipate maoni yao, nimeelimisha sana wasanii wetu wanapozalisha nyimbo zao huzipeleka BASATA na husajiliwa na hupewa maelekezo wimbo gani utatumika wapi na wapi, hatuko hapa kuzuia nyimbo, tuko hapa kutoa muongozo wimbo gani utumike wapi”. ameongeza Dkt. Gwajima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents