Habari

Waziri Mbarawa azindua uhamaji mtandao wa simu bila kubadilisha namba

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa Jumatano hii amezindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana kitaalamu kama (Mobile Number Portability(MNP). Chini ni picha zaidi za uzinduzi huo.

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame M.Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wanaotoa huduma za mawasiliano za simu za mkononi,Watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya sheria wa Vodacom Tanzania,Nina Pendael Eshun,Mara baada ya Waziri huyo kuzindua rasmi huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani inayojulikana kitaalamu zaidi kama (Mobile Number Portability (MNP).Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo jijini Dar es Salaam

 

 

Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame M.Mbarawa akiongea na wadau mbalimbali wa Masuala ya Mawasiliano 
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame M.Mbarawa(kushoto)akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya sheria wa Vodacom Tanzania,Nina Pendael Eshun(kulia) pamoja na wadau wa masuala ya mawasiliano

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents