Habari

Waziri Mwakyembe atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwandishi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepokea kwa mshituko mkubwa taarifa ya kifo cha Mwanahabari na Mpiga Picha mkongwe Ndg. Athumani Hamisi Msengi kilichotokea asubuhi ya tarehe 04 Januari, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Soma taarifa yake;

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa kifo chake ni pigo siyo tu kwa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ambako marehemu aliajiriwa, bali vilevile tasnia nzima ya habari ambayo marehemu alihudumu kwa umahiri wa hali ya juu.

Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia, uongozi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ndugu, jamaa na wanahabari wote nchini na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Kwa kipindi chote cha uhai wake marehemu Athumani amefanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali. Hadi anafikwa na umauti, marehemu Athumani alikuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya HabarLeo.

Imetolewa na:

Octavian F. Kimario
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
06/01/2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents