Burudani

Yamoto Band waeleza sababu ya kuchelewa kutoka kwa video waliyofanya na God Father

Yamoto Band wamesema walikabidhiwa video ya wimbo wake Cheza Kimadoido na muongozaji wa Afrika Kusini Godfather lakini waliomba ifanyiwe marekebisho kadhaa ndio maana imechelewa kutoka.

Yamoto band

Akizungumza na Clouds E ya Clouds TV, mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi hilo, Maromboso amesema kwa sasa video hiyo imekamilika.

“Video ilikuja mara ya kwanza lakini tukasema hapana mbona hiki kipo hivi na hivi, ikapelekwa tena,” amesema. “Lakini sasa hivi imekuja. Mimi kwa upande wangu napenda video nzima, so kuna muda mkubwa alikuja nayo akatuonyesha mara kwanza mara ya pili, yaani tukajikuta tunataka turudie tu. Sasa sijui wananchi wataipokeaje,” aliongeza.

Hata hivyo hakuweza kutaja tarehe rasmi ya kutoka kwa video hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents