Michezo

Yanga yazua gumzo

Baada ya Simba Sc kupoteza dhidi ya Prisons (1-2) na kushinda (1-2) dhidi ya Coastal Union, imeibua moja ya hoja ‘DHAIFU’ kwa baadhi ya Mashabiki maarufu na baadhi ya wachambuzi kwenye media mbalimbali.

Madai makubwa ni kuwa udhamini wa kampuni ya HAIER inayodhamini Klabu ya

, Namungo, Coastal Union inasaidia Yanga kushinda michezo yake kwa kile wanachodai kuwa kuna (CONFLICT OF INTEREST) uwezekano wa kupanga matokeo na kuzipa motisha timu zinazocheza na Simba SC.

Image

Kitu kinacholeta mtafaruku ni baadhi ya wachambuzi wanaaminisha watu kuwa kinachosemwa ndio cha ukweli. Tukienda kwa Hoja. Kanuni na Sheria za (FIFA) na (CAF) hazikatazi kampuni moja kudhamini vilabu tofauti katika Ligi moja.

Image

FIFA inazuia vilabu zaidi ya kimoja kumilikiwa na kampuni au mtu mmoja ndani ya Ligi moja, na wala sio kuzuia Udhamini (SPONSORSHIP). Hili swala la kampuni moja kudhamini timu tofauti katika ligi moja halijaanza leo Tanzania iwaje hoja zinaibuka sasa?
Misimu 3 iliyopita kampuni ya MELT inayomilikiwa na

ilikuwa ikidhamini klabu ya Lipuli na baadae Namungo FC kupitia chapa ya Sabuni ya MO POA, wakati huohuo MELT ilikuwa inaidhamini Simba SC na sio udhamini pekee bali mmiliki kampuni ya MELT

@moodewji alikuwa na hisa.
Kabla ya @moodewji kuwa na hisa 49% Simba alikuwa mmiliki wa klabu ya Africa Lyon, wakati huo akiwa mfadhili wa klabu ya Singida United hoja hizi za sasa wala hazikuibuka muda huo iwaje sasa? Bakhresa kupitia Azam anadhamini vilabu vyote vya ligi kuu na ana timu ya Azam hapo je?
@DStv wanadhamini klabu zote za ligi kuu ya South Africa lakini pia wana timu kwenye ligi hiyo iitwayo Supersport hawa nao hawana fair competition? Vipi kuhusu Vunjabei, Binslum na Sportpesa kudhamini timu zaidi ya 1 kwenye Ligi kuu?

Image

Image

@SimbaSCTanzania– Vunjabei. Prison – Vunjabei. Polisi Tanzania – Vunjabei. Singida Fountain Gate – Vunjabei. Coastal Union – Binslum Tyres. Stand United – Binslum Tyres. Mbeya City – Binslum Tyres. Ndanda – Binslum Vee Rubber. Simba – Sportpesa. Yanga – Sportpesa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents