Burudani

Yemi Alade amwagia sifa Nandy

Msanii wa Nigeria anayetarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta Jumamosi hii ya Novemba 5, Yemi Alade amemsifia Nandy kwa kudai kuwa alitabiri atakuwa msanii mkubwa.

13557058_1621979664760259_2126904976_n

Akiongea mbele ya waandishi wa habari Ijumaa hii wakati wa kuwatambulisha wasanii watakao washa moto kwenye jukwaa la tamasha hilo, Yemi Alade ameisifia video mpya ya msanii huyo ‘Nagusagusa’ na kusema kuwa alijua tangu mwanzo muimbaji huyo atakuwa ni msanii mkubwa kwa kuwa alishawahi kumuona kwenye mashindano ya kutafuta vipaji ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.

Nandy ni msanii mmoja wapo aliyechaguliwa kuwasha moto kwenye tamasha hilo, wasanii wengine ni pamoja na Weusi, Maua Sama, Navy Kenzo, Alikiba, Mr Blue, Rayvanny, Darassa, Jay Moe, Barakah The Prince, Bill Nas, Fid Q, Belle 9 na wengine.

img_4247
Tekno, Yemi Alade na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Fleva wakiongea na waandishi wa habari

Wasanii wengine kutoka nje ya Tanzania ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo ni pamoja na Tekno (Nigeria) na Chameleon (Uganda).

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents