Michezo

Zaza nitafanya vizuri ndani ya klabu ya Valencia

Mchezaji ambaye amesajiliwa hivi karibuni na klabu ya Valencia, Simone Zaza amesema anaamini kutua kwake katika kikosi hicho ni sehemu ya kurejesha heshima yake.

Zaza ambaye ni raia wa Italia amesema ndani ya Valencia ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa kuwa ni sehemu ambayo atatulia.

“Sihitaji kitu zaidi ya upepo, ufukwe na bahari ya Valencia. Ni eneo zuri la kuishi, ninaamini nitafanya kazi yangu vizuri,” alisema.

Zaza ambaye alishindwa kufanya vizuri alipokuwa akikipiga katika klabu ya West Ham United ya Uingereza ambayo alijiunga nayo akitokea Juventus.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents