Habari

Zitto Kabwe apokelewa Z’bar na mamia ya watu, Maalim Seif amkaribisha kwa maneno mawili (+video)

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe leo Machi 21, 2019 amepokelewa na mamia ya wanachama wapya wa Chama hicho visiwani Zanzibar.

Zitto amekaribishwa na mwenyeji wake, Maalim Seif, katika ofisi mpya za ACT- Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja ambazo awali zilikuwa makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) visiwani humo.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo majira ya saa 4 asubuhi, Maalim Seif alimpokea Zitto huku mamia ya wanachama wapya wa ACT- Wazalendo wakimpokea kwa nyimbo mbali mbalimbali zikiwemo za chama hicho.

Wote wawili Zitto na Maalim walivalishwa mataji kama heshima na baadae walipewa nafasi ya kuzungumza kwa ufupi.

Zitto alipewa nafasi ya kwanza kuzungumza ambapo alisema “Nina furaha sana leo, nataka kuwahakikishia tumeshashusha tanga, tumeshapandisha tanga, safari inaendelea.”. Huku mwenyeji wake Maalim Seif aakimkaribisha Zitto kwa maneno mawili “ACT-Wazalendo…?” huku wanachama wapya wakishangilia kwa kumjibu “Taifa Kwanza”.

Mnamo tarehe 18 Machi mwaka huu, Maalim Seif pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa CUF, walikabidhiwa kadi za uanachama wa ACT- Wazalendo katika shughuli iliyofanyikia makao makuu ya ACT- Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents