Burudani

Zodiac Party: Team Aries kusherehekea siku zao za kuzaliwa Club 327, Dar

Jumamosi hii (March 22) pale Club 327, ndipo watakutana wana Aries kusherehekea birthday zao. Aries ilitangazwa rasmi kwamba itakuwa sherehe ya kwanza kuanza kwa mwaka na kufuatiwa na nyota nyingine.

zodiac

Akiongea na Bongo5, Nadia Taylor ambaye ni mmoja wa waratibu wa show hiyo amesema party hiyo itakuwa ya kipekee na kwamba watakaoingoza ni watu mashuhuri nchi ambao nao ni Team Aries.

“Japo kuna watu wamekuwa wakiniuliza ni Abby?! nabaki kuwashangaa kwasababu theme ya celebrations zetu ni surprise, yaani hakitangazwi kitu mpaka siku yenyewe utakayojionea kwamba ni kweli Abby wa Big Brother ama vipi,” amesema.

“Unajua tumeshazoea events ambazo unaambiwa kutakuwa na fulani fulani sasa hii ya kwetu haiko hivyo ni tofauti, yani tunakuacha wewe uingie ndani na ujionee wewe kila kitu, si unajua surprise zinavyokuwa tamu, ni raha tu yani kama AY anavyosema. Ila Jumamosi hii usiku weka kwenye ratiba yako kabisa ni muda wa wana Aries kucelebrate ni official pale club 327 sikushauri kukosa kwasababu the entrance fee is fair ni elfu kumi tu lakini utapata mengi sana ya kusimulia baada ya kutoka hapo.”

Zodiac Entertainment ni kampuni inayojishugulisha na uandaaji wa events mbalimbali lakini kubwa zaidi ni series za zodiac signs.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents