Burudani

Afande Sele: Darassa kawafunga mdomo waliosema hip hop imekufa!

Afande Sele katupa jiwe gizani ama kalitupa kwa hasimu wake Madee? Vyovyote vile, Mfalme huyo wa Rhymes amempongeza rapper Darassa kwa kumuelezea kama mtu aliyekuja kuwafunga mdomo watu waliowahi kudai kuwa hip hop imekuja – au kama ambavyo Madee aliwahi kusema ‘hip hop haiuzi.’

14374253_102020210266220_6492267028420755456_n

Kauli yake inakaribisha mjadala mwingine mrefu na ambao ni ngumu kupata mshindi kuhusu iwapo anachofanya Darassa sasa ni hip hop!

Kupitia Instagram, Afande ameandika:

Mtu yeyote anaetumia AKILI katika jambo lake mara nyingi hufikia malengo…wapo madogo zangu wengi wakali sana…mimi wote nawakubali lakini umuhimu wa kipekee nampa @darassacmg ‘El Classico Darasa’ leo hii ni kwa sababu kaja kukanusha uzushi na upuuzi wa kuiaminisha jamii kwamba hiphop imekufa kiasi cha wengine kuthubutu kuinajis hiphop kwa kuilinganisha na singeli…Roho saba katika moja ya mistari yake ndani ya wimbo Nakupenda hiphop anasema’Hiphop ndio mziki na hili lake biti…Amba nipe kiki niwabastie mamluki….Nakupenda Hiphop…Nakuheshimu @darassacmg ….Here we go bro….

Darassa amekuwa kwenye headlines tangu aachie wimbo wake Muziki unaoaminika kuwa ndio wimbo namba 1 Tanzania kwa sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents