Habari

Baba mzazi wa Akwelina awaomba kitu Watanzania, Waziri Ndalichako atangaza neema

Safari ya mwisho ya mwili wa mwanafunzi, Akwelina Akwilini aliyepigwa risasi Februari 16, 2018 hatimaye imefika mwisho leo Ijumaa ya Februari 23, 2018 kwa kuzikwa huko Rombo mkoani Kilimanjaro.

Wazazi wa Akwelina wakiweka mashada kwenye kaburi la mtoto wao

Baadhi ya vitu vilivyopokelewa kwa faraja katika familia ya Mzee Akwilini ni ahadi ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ya kumsomesha mdogo wa marehemu ambaye awali alikuwa anasomeshwa na Akwelina kwa fedha za mkopo wa Chuo.

“Binti huyu ambaye tumempumzisha kwenye nyumba yake ya milele alikuwa anapambana katika kusaka elimu ili aweze kuikwamua familia yake nimesikitika pia kuona kwamba pamoja na fedha zile ambazo Akwelina alikuwa anapata kwa ajili ya yeye kujikimu lakini alikuwa anatumia fedha hizo hizo kumsaidia mdogo wake Angela ambaye yupo kidato cha tatu naomba nisema kwamba huyo binti Angela nitamchukua kwa sababu natambua na kuthamini elimu hivyo nitahakikisha kwamba namsomesha mpaka uwezo wake na ndoto zake zitakapofikia,”amesema Prof. Ndalichako wakati wa kuuaga mwili wa Akwelina.

Waziri Ndalichako akitoa pole kwa wazazi wa Akwelina

Kwa upande mwingine, Baba mzazi wa Akwilina akiongea na Bongo5 baada ya kutoka makaburini ameishukuru Serikali pamoja na Watanzania waliojitokeza katika kuuaga mwili huo, huku akiwaomba Watanzania kuendelea kumkumbuka kadri wawezavyo kwani ili kuifariji familia yake.

Hata hivyo mama Mzanzi wa Marehemu Akwilina alipohojiwa na Bongo5 ameshindwa kuongea huku machozi yakimtoka kwa uchungu wa mwanaye.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents