Bongo Movie

Baba mzazi wa Lulu afunguka mwanaye kuolewa, ‘sitaki posa’

Baba mzazi wa msanii wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mzee Kimemeta amefunguka mambo kadhaa kuhusu mwanaye kuolewa.

Akizungumza na East Africa Radio, Mzee Kimemeta amesema kwanza hana shinikizo kwa mwanaye aolewe na mtu fulani kwa sababu ni maarufu bali ni maamuzi yake binafsi na suala la posa kwake halipo.

“Suala la kuoana mimi halinihusu ni suala la watu wawili, anayeoa na anayeolewa, yeyote atakayemleta akaniambai baba huyo ndio wangu sisi tunambariki” amesema.

“Hapa, sisi kwa kweli posi haipo katika msamiati wangu, siuzi mtoto wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea,” amemaliza kwa kusema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents