Siasa

Balozi Wa Brazil Alonga

Balozi anayeiwakilisha Brazil nchini Tanzania bwana Francisco Carlos Soares Luzleo asubihi amenena kuwa hakuamini kwa mara ya kwanza kuwatimu ya taifa ya Brazil ilikuwa inakuja Dar-Es-Salaam katika mechi ya kujipima nguvu kabla ya kuanzarasmi michuano ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini hapo tarehe 11 mwezi wa 6 mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari wa Redio Clouds Fm katika kipindi cha asubuhi “ Power Breakfast” balozi Francisco Carlos Soares Luz alisema “ nilipigiwa simu na mwandishi wa gazeti la the Citizen akiniuliza kuhusiana na ujio wa timu ya taifa langu.kwa kweli sikuwa na taarifa hizo na wala sikuwa nategemea suala hilo kutokea.

Ilinibidi kuwasiliana na watu mbalimbali nyumbani Brazil na baada ya siku kadhaa nilipata uhakika wa kuwa timu ya taifa ya Brazil inakuja kucheza mechi moja na Taifa Stars. Kusema ukweli nilifarijika na kujisikia furaha kupata habari hizo.

Akiendealea kuelezea balozi anasema mchakato wa ujio huo wa timu ya Taifa ya Brazil Tanzania ulifanywa siri kubwa kati ya mashirikisho mawili ya mpira ya Tanzania na brazil kwenyewe.

Akijibu swali kuhusu ni kwa jinsi ganiwabrazil pamoja na yeyewaishio Tanzania wamepokea habari hizo Balozi alijibu “ kwa kweli naisubiri siku hiyo kwa hamu na shauku kubwa kwani naelewa kuna wabrazil ya pata 50 hivi waliopo hapa nchini. Kuna baadhi wapo hapa Dar-Es-Salaam na wengine wapo Morogoro, Mbeya na Mtwara.

Wote kwa pamoja hii ni nafasi yao nzuri ya kushuhudia mahusiano mazuri ya kitamaduni kati ya watu wan chi hizi mbili. Mimi pia naisubiri siku hiyo kwani itakuwa faraja kwangu kukaa uwanjanina mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais kikwete tukiangalia mchezo huo

Pia nina habari kuwa kuna raia wengine wa Brazil watakaokuja Tanzania kuangali mechi hii kati ya Tanzania na Brazil ambao wanatoka Nairobi Kenya , Angola na Mozambique. Tayari shirika la ndege la Mozambique limeongeza safari zake za kuja nchini Tanzania ikiwaleta watu hawa ku ushuhudia mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira huo katika ukanda huu wa Africa Mashariki na zaidi.

Haya sasa Wapenzi wa soka

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents