Michezo

Bingwa wa riadha wa Olyimpiki Kenya akutwa na hatia nzito

Bingwa wa Olyimpiki wa mbio za masafa marefu upande wa akina dada marathoni, Mkenya Jemima Sumgong, amepigwa marufuku ya kutoshiriki shindano lolote kwa muda wa miaka minne, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli michezoni.

Kwa mujibu wa shirikisho la riadha nchini Kenya-AK, Sumgong ataanza kutumikia adhabu hiyo kuanzia mwezi April mwaka huu wakati aliposimamishwa kwa muda.

Sumgong ni mwanariadha wa pili wa ngazi ya juu mwanamke kupata adhabu kama hiyo, baada ya bingwa wa mbio za New York na Boston Rita Cheptoo kupigwa marufuku pia.

Bi Sumgong ni mwanariadha wa Kwanza wa Kenya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathoni za Olyimpiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents