Tia Kitu. Pata Vituuz!

Bongo movies na Wanamuziki leo kufanya mikutano muhimu

Jumatano ya leo kunafanyika mikutano miwili muhimu ya tasnia ya burudani nchini.
Mkutano wa kwanza ni wa wasanii wa muziki walio na mkataba na kampuni ya Push Mobile kuhusiana na masuala ya ringtone.
Mkutano huo ulioitishwa na kampuni hiyo unafanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Push Mobile lengo la mkutano huo ni kutoa msimamo na kupokea maoni juu ya biashara ya ringtone.
Nao Waigizaji, waongozaji, wasambazaji na wadau wengine wa filamu nchini wanaendesha mkutano wao utakaofanyika kwenye viwanja Leaders Club ambapo kutakuwa na mambo mbalimbali ya yatakayojadiliwa.
Makundi yanayotarajia kuwepo katika mkutano huo ni waigizaji, watayarishaji wa filamu, waongozaji wa filamu, waandishi wa muswada, walimu wa vikundi vya sanaa, watafuta mandhari, wapiga picha za filamu, wapambaji, wasambazaji, wachekeshaji, na wadau wa filamu kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW