Siasa

BoT yajitokeza kumsafisha Balali

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema hali ya afya ya Gavana wa benki hiyo, Bw. Daudi Balali inaendelea vizuri katika hospitali ya Boston Massachusetts nchini Marekani, ambako amelazwa.

Na Joseph Mwendapole



Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema hali ya afya ya Gavana wa benki hiyo, Bw. Daudi Balali inaendelea vizuri katika hospitali ya Boston Massachusetts nchini Marekani, ambako amelazwa.


Vile vile, imekanusha madai kuwa Bw. Balali, amendika barua ya kujiuzulu wadhifa wake.


Mkurugenzi katika ofisi ya Gavana, Bw. Joseph Mhando, alisema jana katika taarifa yake kuwa hawajapata taarifa rasmi ya kujiuzulu kwa Bw. Balali.


Bila kutaja ugonjwa unaomsumbua Bw. Balali, Bw. Mhando alisema Gavana huyo alikwenda nchini humo kwa matibabu tangu mwezi Agosti mwaka huu na mpaka sasa anaendelea na matibabu.


“BoT haijapata mawasiliano yoyote rasmi kuwa Bw. Balali amejiuzulu wadhifa wake“. Tunachotambua ni kuwa Bw. Balali bado ni bosi wa taasisi hii,“ alisema.


Aliongeza kuwa gharama za matibabu za Gavana huyo zinatolewa na BoT kwa kushirikiana na bima yake binafsi ya afya.


Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti hivi karibuni kuwa Bw. Balali alimwandikia barua Rais Jakaya Kikwete akiomba kujiuzulu.


Hata hivyo, baada ya habari hizo kutoka, Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Bw. Salva Rweyemamu, ilikanusha uvumi huo.


Bw. Rweyemamu alisema yeye binafsi ameshangaa kusikia habari hizo kwenye vyombo vya habari huku vingine vikidai kuwa vina nakala ya barua aliyoiandika.


Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji, naye alisema hajapata taarifa zozote za kujiuzulu kwa Bw. Balali.


Vyama vya upinzani navyo baada ya kusikia uvumi huo vilimuomba Rais Kikwete kukataa ombi la Bw. Balali la kutaka kujiuzulu vikidai kuwa kuna usanii unataka kufanyika.


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents