Siasa

Bunge la Kumi lazinduliwa rasmi

 

Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, jana lilizinduliwa rasmi kwa mara ya kumi katika makao makuu ya nchi, Dodoma na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Shughuli hiyo ilifanyika majira ya saa kumi jioni ambapo spika wa bunge hilo Anna Makinda alimuongoza Rais Kikwete ukumbini hapo, na kutanguliz shughuli kwa sala ndipo Mh. J.K aliwasilisha hotuba yake.

Kwa kile kilichoonekana kuwa jambo la kustaajabisha, ni wabunge wa Chadema kunyanyuka na kuondoka ukumbini hapo punde tu rais aliponyanyuka kuhutubia,kana kwamba hawamtambui kiongozi huyo wa nchi. Hatua hiyo ya wabunge hao iliwaacha wengi katika mshangao ukumbini hapo.

Rais Kikwete aliendelea na uzinduzi huo kwa kutaja yale aliyodhamiria kuyanfanya kwa muda wake huu unaomalizikia, kuwa yale ya kuboresha miondomibinu, kunyanyua sekta ya elimu, makazi, kilimo na uchumi wa nchi yetu.

Kila La Kheri.

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents