Burudani

Chris Brown amgalagaza ‘baby mama’ mahakamani

Chris Brown anasherehekea ushindi baada ya kumlagaza mama wa binti yake Royalty mahakamani.

0812-chris-brown-nia-guzman-instagra-facebook-4

Nia Guzman alikuwa akitaka apewe haki ya kuishi na mwanae muda wote, ombi lililokataliwa. Pia alitaka Chris awe na uangalizi awapo na mtoto wao, ombi lililokataliwa, kwa mujibu wa TMZ.

Pia alitaka kukatazwa kwa mama yake Chris asimuone mjukuu wake, ombi lililokataliwa na kama haitoshi alitaka Chris awasilishe vipimo vya matumizi ya madawa, ombi lililokataliwa pia.

Jaji alimwachia Chris haki ya awali ya kukaa na mwanae kwa siku 12 ndani ya mwezi.

Pindi Nia alipowasilisha mashtaka yake, jaji alimwagiza Chris ampe $20k ili amudu gharama za wanasheria. Lakini jaji alidai Nia hana haki ya kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Kama haitoshi Nia alitaka alipwe $16k kutoka $2,500 anayolipwa sasa, kitu ambacho jaji amekikataa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents