Michezo

Chuji apata shavu Ndanda FC

Kiungo wazamani wa  Yanga SC, Athumani Iddi ‘Chuji’ amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ya kuitumikia klabu ya Ndanda FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Chuji sasa ataitumikia Ndanda FC ya mkoani Mtwara ambayo imeonekana kusuasua msimu uliopita.

Mwaka 2009 ambapo kiwango cha mchezaji huyo kilipo onekana kushuka aliingia katika matatizo na kocha Maximo katika timu ya taifa na klabu yake, Dusan Kondic, lakini bado walikuwa wakisema kuwa hakuna kiungo kama Chuji katika nyakati za sasa nchini.

Juhudi kubwa zimefanywa na Chuji katika kuhakikisha anarejea katika Ligi Kuu ya Vodacom na siku za hivi karibuni ameoneka kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Ndondo FC.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents