Diamond aiachia video ya ‘Ntampata Wapi’ MTV Base na vituo vingine vya nje!

Diamond Platnumz jana aliachia video ya wimbo wake mpya ‘Ntampata Wapi’ kupitia MTV Base na vituo vingine vya runinga vya nje. Video hiyo iliyoongozwa na Godfather Productions, ina hadithi inayoweza kuwa na maana nyingi.

10378252_833977959957353_2677925388952221456_n

Kuna scene yenye watu wengi wakiwa kwenye sherehe ambapo Diamond anaonekana akipiga violin na mrembo mmoja mwenye gauni jekundu kumzimikia. Diamond anapata nafasi ya kucheza muziki na mrembo huyo. Diamond anakuwa pamoja na msichana huyo ambapo kuna sehemu anaonekana akimchora picha yake na kufurahi pamoja.

928828_770004943054671_70461098_n

Licha ya msichana huyo mrembo kumpenda staa huyo, script inampa mtazamaji wa video tafsiri mbili. Ya kwanza anapata vishawishi vingi vya kuwa na mwanaume (mtu mzima) mwenye fedha nyingi anayemnunulia vitu vya thamani ikiwa ni pamoja na magari. Lakini pia huenda mzee huyo anaweza kuwa ni baba yake anayempenda mno binti yake kiasi cha kuwa karibu naye muda wote na hivyo kumnyima nafasi Diamond ya kuwa naye atakavyo. Kuna scene ambayo mzee huyo anamzawadia binti yake Lamborghini.

Kuna scene wanaonekana wakiwa pamoja kitandani wakifurahi pamoja na kisha Diamond kuamka na kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni ndoto tu.

10748491_1741409226084632_1583228381_n

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW