Bongo5 Exclusives

Exclusive: Show ya Nas na Damian Marley Dar yaahirishwa hadi June au September

Nas+Damian+Marley+Coachella+Valley+Music+Arts+2jBBfnuoPs2l

Hivi karibuni tuliandika habari kuhusu ujio wa rapper Nas na mtoto wa mwisho wa hayati Bob Marley, Damian Marley nchini Tanzania ambapo kwa mujibu wa ratiba ya awali show ilikuwa imepangwa kufanyika leo.

Baada ya kuona kimya tumewasiliana na mratibu wa show hiyo aitwaye Kiya ama Rouqayyah Omusigyi’Omukungu Nyabingi kama anavyojulikana kwenye mtandao wa Facebook kutaka kujua kama ujio wa mastaa hao umefikia wapi. Kiya amesema ziara hiyo imeahirishwa kwasababu mapromoter bado hawajalipa hela na hivyo wameisogeza hadi mwezi June ama September mwaka huu.

Kiya ambaye ni mwanzilishi na balozi wa kampuni ya T W Rhino: True Wise Rhino Village ametujibu kupitia Facebook kwa kuandika, “Greetings, that was initially the plan, BUT promoters have not paid up, so we have re-scheduled the whole Tour for between June and September.”

nas

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents