Bongo5 ExclusivesVideos

Exclusive Video: 1 on 1 with Anisa Mpungwe – Tanzanian-born, South Africa-based designer

Anisa Ami Mpungwe ni mbunifu maarufu wa mavazi aliyezaliwa nchini Tanzania na kuhamia nchini Afrika Kusini akiwa na miaka kumi.

Amesoma nchini Afrika Kusini hadi chuo kikuu na baadaye kwenda kuongeza elimu nchini Uingereza. Ana fashion label maarufu nchini Afrika Kusini iitwayo Loin Cloth and Ashes. Ameshawavalisha watu maarufu duniani wakiwemo Oprah, Michelle Obama, Solange Knowles na wengine.

Nov-cover-Small
Solange, mdogo wake Beyonce akiwa kwenye kava la jarida la Elle la Afrika Kusini. Nguo alizovaa zilitengezwa na Anisa Mpungwe

Akiongea kwenye mahojiano maalum na Bongo5, Anisa amesema haikuwa kazi rahisi kuwashawishi wazazi wake kusomea masomo ya fashion kwakuwa baba yake alikuwa akipenda asomee masuala ya ubinufu wa vito vya madini nchini Marekani lakini yeye akasisitiza angependa kusoma huko huko Afrika Kusini na kujihusisha zaidi na fashion.

Mwaka 2008 Anisa alikuwa Mwaafrika Mweusi wa kwanza kushinda shindano la Elle New Talent lililomweka kwenye ramani ya kiwanda cha fashion nchini Afrika Kusini.

“Nilioomba kushiriki kwenye shindano hilo na nikawa miongoni mwa watu sita waliongia fainali,” amesema. Amedai kuwa takriban watu 1000 walishiriki nchi nzima na yeye kuibuka mshindi na hivyo kupata nafasi ya kutengeneza nguo kwaajili ya maduka ya Mr Price.

Solange-in-action

“Jaribu kufikiria matangazo ya msichana huyu mwenye miaka 22 ni kitu kikubwa. Idadi ya nguo unazotengeneza ni kama maelfu, laki na kila mtu nchi nzima atakuwa akizivaa. Kwahiyo ni shindano zuri la linakufunza kuhusu biashara.”

The-Hair

Anisa amesema baada ya miaka minne baada ya kufungua duka lake na jina lake likiwa maarufu tayari, aliombwa na waandaji wa shindano hilo kuwa jaji na wakati mmoja alikuwa akitaniana na mmoja wa watu wa Mr Price kuwa kwakuwa jina lake ni kubwa ni vyema wakifanya tena kazi pamoja.

anisa-mpungwe-for-mr-price-pricest-at-sandton-city-store-mj-and-stufd
Nguo za Anisa zikiwa kwenye duka la Mr Price huko Sandton, Afrika Kusini

“Kumbe walichukulia serious hivyo walinipigia mwezi mmoja baadaye na wakasema ‘Anisa Let’s do this, let’s do another collection’.

Mwaka huu Anisa ametajwa kuwania tuzo za MTV MAMA kwenye kipengele cha ‘Transform Today Award by Absolute.

BoD8cMYIIAAEa6H

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents