Michezo

Gonzalo Higuain afungiwa mechi nne kwa kosa la kumsukuma mwamuzi

Mchezaji wa klabu ya Napoli, Gonzalo Higuain amefungiwa mechi 4 kwa kosa la kumsukuma mwamuzi katika mchezo dhidi ya Udinese uliofanyika jumamosi iliyopita.

TURIN, ITALY - MARCH 17: Gonzalo Higuain of SSC Napoli celebrates after scoring the opening goal during the Serie A match between Torino FC and SSC Napoli at Stadio Olimpico di Torino on March 17, 2014 in Turin, Italy. (Photo by Valerio Pennicino/Getty Images)

Mbali ya Kifungo cha michezo hiyo 4 mshambuliaji huyu, ametozwa faini ya kiasi Euro 20,000.

Katika mchezo huo Higuian alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata Kadi za Njano ya Pili kwa kumcheza faulo Felipe wa Udinese.

Kukosekana kwa mshambuliaji huyo kutoka Argentina ni pigo kwa Napoli ambao wanagombea Ubingwa wa Italy wakiwa na alama 6.

Adhabu hii itamfanya Higuian kukosa michezo dhidi ya Verona, Inter Milan, Bologna na ule wa As Roma.

Sorce: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents