Burudani ya Michezo Live

Habari zilizowahi kuwashika wengi siku ya wajinga duniani, Tanzania na duniani kote

Wewe ni miongoni mwa watu waliowahi kuambiwa jambo la uongo kwenye siku hii na ukaamini kiasi cha moyo wako kutaka kutoka nje kwa wasiwasi ama furaha? Hauko peke yako. Hizi ni habari zilizowahi kutangazwa kwenye siku ya wajinga duniani na kuwashika maelfu ya watu.

DUNIANI

Miti ya Tambi

Spaghetti tree

Huu ni uongo uliotikisa mwaka 1957 uliotangazwa kwenye kipindi cha Panorama cha BBC.
Ilikuwa ni habari ya dakika 3 kuelezea kuwa kuna uvunaji wa ‘tambi’ ama spaghetti huko kusini mwa Switzerland. Habari hiyo ilionesha kipande cha video pia kinachoonesha familia ikivuna tambi kutoka kwenye miti na kuweka kwenye vikapu.

Miongoni mwa wale waliokamatwa na uongo huo ni aliyekuwa mkurugenzi wa BBC Ian Jacobs, aliyekiri kuangalia “spaghetti” kwenye encyclopedia yake.

Mamia ya watu walipiga simu BBC kutaka kufahamu kama wanaweza kupanda miti yao ya tambi. Kujibu swali hili BBC ilisema: “Place a sprig of spaghetti in a tin of tomato sauce and hope for the best.”

Matangazo ya TV yenye rangi

April-Fools--Colour-TV-1790185

Nchini Sweden mwaka 1962, kulikuwa na kituo kimoja tu cha runinga na kilikuwa kinaonesha kwa black and white. Kituo hicho kilitangaza kuwa mtalaam wake wa ufundi Kjell Stensson, alikuwa anaenda kuwaambia watazamaji jinsi ya kuona picha za rangi kwenye tv zao black-and-white.

Alisema alikuwa amegundua kuwa kwa kuifunika tv kwenye pair za tights ama nguo zinazobana zingesababisha mwanga upinde na kuzifanya picha zionekane na rangi. Watazamaji wote walifanya hivyo kwa kuzikata kata socks ama nguo zingine za kubana na kuzibandika kwenye tv.

Maelfu ya watazamaji waliingizwa mkenge. Wengi wanasema leo kuwa wanakumbuka wazazi wao hasa baba zao walivyohangaika kutafuta nguo hizo kufunika TV zao. Matangazo ya TV ya rangi nchini Sweden yalianza April 1, 1970.

Pluto na Jupiter kusogeleana na kusababisha athari ya nguvu ya mvutano kwenye dunia

Artists-impression-of-the-planet-Kepler-37b-1720446

Wakati wa mahojiano kwenye kituo cha BBC Radio 2, asubuhi ya 1 April 1976, mnajimu Patrick Moore alitangaza kuwa itakapofika saa 9:47 AM tukio kubwa la kinajimu lingetokea ambapo sayari ya Pluto ingekatiza nyuma ya Jupiter na kusababisha kwa muda mabadiliko ya nguvu ya mvutano na kupungumza mvutano kwenye dunia. Moore aliwaambia wasikilizaji kuwa kama wakiruka hewani muda huo wangehisi kama wanaelea hewani.

BBC ilipokea mamia ya simu kutoka kwa wasikilizaji wakidai kuhisi kitu kama hicho. Mwanamke mmoja alidai kuwa yeye na marafiki zake 11 waliinuliwa kwenye kiti na kuelea hewani kwenye chumba walichokuwa wamekaa.

Burger special kwa watu wanaotumia mkono wa kushoto

Burger King Whopper Cheeseburger with tomato lettuce and mayonnaise on bun

Burger King walichapicha ukurasa mzima wa tangazo kwenye gazeti la USA Today mwaka 1998. Tangazo hilo lilidai kuwa kuna msosi mpya kwenye menu yao, Burger maalum ya watu mashoto (Left-Handed Whopper).

Ilikuwa imetengenezwa mahsusi kwa wamarekani milioni 32 wanaotumia mkono wa kushoto. Maelfu ya wateja walienda kwenye mgahawa kuagiza burger hiyo huku wengine wakiomba kuwepo version nyingine ya wanaotumia mkono wa kulia.

Mashine ya kutengeneza chakula

Gazeti la Marekani The Daily Graphic liliandika habari mwaka 1878, kuhusu ugunduzi wa aina yake. Thomas Edison alikuwa amegundua “the Food Creator… mashine ambayo italisha wanadamu kwa kutengeneza nyama, mboga, mvinyo na biskuti kwa kutumia hewa na maji.

TANZANIA

Wakazi wa Dar wadanganywa kupata huduma za Babu Loliondo

DSC00998

Habari hii iliwashika wengi hasa kwakuwa iliandikwa kwenye kipindi ambacho Babu wa Loliondo alikuwa juu na wengi walikuwa wanatamani kwenda kupata tiba yake. Wakati huo safari ya kwenda Loliondo haikuwa rahisi kutokana na magari mengi kuelekea huko.

Habari hiyi iliyoandikwa April 1, 2011 ilisomeka: HATIMAYE Mchungaji Ambilikile Masapila ‘Babu’ amelegeza msimamo wake wa kukataa kuhama katika Kijiji cha Samunge ili kupata sehemu ya wazi ambako atatoa huduma bila msongamano na sasa amekubali ombi la kutoa tiba katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.

Hatua hiyo ambayo imepokewa kwa shangwe na wakazi wa Dar es Salaam na mikoa jirani, imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Babu na viongozi wa serikali, kutokana na maombi ya kumtaka mchungaji huyo ahamie sehemu ambayo itakuwa rahisi kufikika ili kuepuka maafa zaidi.

Mwisho liliandika: Babu Masapila aliwaomba wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi na kuwahi, bila kujali kuwa leo ni Siku ya Wajinga.

Michuzi awakamata wasomaji wake kuwa amepata shavu VOA

DSC_8182

Mwaka 2011 Michuzi alifanikiwa ipasavyo kuwaingiza mkenge wasomaji wa blog yake baada ya kuandika habari yenye picha kuwa amepata shavu la kuwa mtangazaji wa Voice of America na atakuwa anaripoti kutoka Ikulu ya White House. Alidai kuwa amechukuliwa kuziba pengo la Juma Nkamia ambaye kwa sasa ni mbunge.

“Ameiambia Globu ya jamii kwamba anamshukuru Mungu kwa kudakwa VOA na hivi sasa anajiandaa kupigana vikumbo na wanahabari wa dunia. Kasema ana uhakika kwmaba endapo hayatakuwa mswano ataingia mtaani kubeba boksi,” ilisomeka habari hiyo.

Habari hiyo ilipata comments 310 huku wengi wakimpongeza Michuzi kwa shavu hilo. Wachache lakini walishtukia kuwa ilikuwa ni habari ya siku ya wajinga duniani.

Ebony FM kufungwa

Mwaka 2010 kituo cha radio cha Iringa Ebony Fm kilitoa habari iliyowasikitisha wapenzi wake kuwa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, iliagiza kituo hicho kufungwa majira ya saa 6 mchana kwa sababu zisizo julikana.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa masikitiko makubwa na wadau wa radio hiyo huku baadhi yao wakikdai kuwa uwazi wa Radio hiyo katika kuibua kero za wananchi na vitendo vya ufisadi ndio ambao umeiponza.

Wengine walidai kuwa hakuna radio ambayo itaweza kufikia hatua iliyofikiwa na Radio Ebony Fm katika kuwaunganisha wananchi na vyombo vya habari na kutumia vyema uhuru wao wa kutoa maoni yao.

Gaddafi akimbilia Tanzania

Habari hii iliandikwa na gazeti la The Citizen kipindi ambacho kiongozi huyo wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi alikuwa anatafutwa na vikosi vya NATO.

Citzen iliandika: Impeccable sources said that Col Gaddafi had escaped from Tripoli in a private jet that landed at the Julius Nyerere International Airport under the cover of darkness last night.He was soon whisked away and was spotted by our team in one of the five-star hotels in the city centre, where security cordon was immediately thrown.

With him were scores of close family members and aides, including a team of his familiar heavily armed, high-heeled female bodyguards. The embattled leader apparently violated the non-fly zone imposed by Nato over Libyan, and made his daring escape.

It wasn’t clear why he chose Tanzania for refuge, but sources in the government team assigned to him revealed that his second wife, Safia al-Gaddafi, was the one who had convinced them to seek refuge in the city popularly known as the Haven of Peace.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW