Uncategorized

IGP Sirro awashangaa askari wasiotoa dhamana siku za Jumamosi na Jumapili!

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro amewataka askari kufuata maadili yao ya kazi pamoja na kuacha kuwaweka maabusu watu ambao wanaweza kupewa dhamana kama sheria inavyotaka.

IGP Siro ametoa kauli hiyo akiwa Jijini Arusha akitokea Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo.

“Asiyetoa dhamana kwa makosa ambayo ni ya dhamana kwa siku za Jumapili au Jumamosi …au anasema ni usiku sana, huyo hajui wajibu wake,”

Siku chache zilizopita Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola alikemea utaratibu wa watuhumiwa kunyimwa dhamana hasa siku za mapumziko kwa kisingizio kuwa si siku za kazi.

Amesema dhamana ni haki ya mtu endapo kosa lake  linadhaminika huku akiwataka wananchi watakaoombwa fedha ili wapewe dhamana kuripoti tukio hilo kwa maofisa wa ngazi za juu ili askari husika achukuliwe hatua za kinidhamu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents