Diamond PlatnumzUmbea

Its Official: Diamond confirms He and Jokate are an Item.

Baada ya Speculation ya muda mrefu, Diamond Platnumz amekiri wazi penzi lake kwa Jokate Mwegelo, ambaye kwa muda mrefu alikua amekataa kudhibitisha uhusiano wake na yeye.

Diamond, kupitia Blackberry messenger status yake amekiri kumpenda Jokate kwa kuweka picha ya Jokate na kuambatanisha status message iliyosema,

“I love you Kate and there is no one like u in ma life”

‘Baada ya lisaa limoja Diamond alibadili tena status yake na kuweka ishara ya busu kwa mpenzi wake huyo Jokate.

Inasemekana kwamba Diamond na Jokate walianza uhusiano wao wakati Diamond bado akiwa anatoka na Wema Sepetu ambapo ikampelekea Wema kumtaja Jokate kwenye vyombva vya habari kwamba ndiye anayemharibia uhusiano wake na Platnumz. Wawili hao walikana uhusiano wao mara kwa mara, ingawa ishara zote zilionyesha ukweli wao na kwa kua mapenzi ni kikohozi na kulificha huliwezi, hatimaye penzi limefichuka.

Itakumbukwa kwamba Diamond,ambaye anaonekana kuwa hoi kwenye mapenzi na Jokate,aliwahi kufanya video na Kate, ya wimbo wake wa ‘Mawazo’na pia alishuka na demu wake huyo pamoja na mama yake kwenye gari moja katika show yake ya ‘Diamonds are forever’ Mlimani City ambapo Diamond alimsusia ex wake Wewma ambaye alienda kumtunza pesa stejini huku Jokate na Rafiki Zwake wakishangilia tukio hilo.

Diamond akicheza na Jokate

Jokate pia amekua mstari wa mbele katika kumtengenezea mzee wake mavazi tofauti kupitia brand yake mpya ya Kidoti, kama invyoonekana kwenye picha hizi wakiwa kwenye fashion show ya Tanzania Mitindo House, ambapo Diamond alikua show stopper Model wa Jokate na kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Awards ambapo Diamond, alipokua amanapokea tuzo yake ya Video bora ya mwaka, pia alirock kitu cha Kidoti cha Mamsup!

Diamond akiwa amevaa design ya Jokate

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents