Bongo5 Makala

Kalamu ya Nick wa Pili: Hip hop inavyoikwamisha hip hop Tanzania

Hip hop kwa upande wa kwanza ni CNN,BBC ama TBC (Sauti) ya mageto na mitaa mara nyingi ya watu wa chini. Na sehemu ya pili ni fursa ya kuwatoa vijana magetoni na familia zao pia. Mfano akina Jay Z, Luda, Eminem, Kanye, hawaishi tena kitaa ni matajiri wakubwa.

Nikki  wa Pili na Stamina

Hip hop Tanzania katika upande wa sauti ya mtaa imefanya kazi kubwa sana, toka nyimbo kama Dei Waka, Mikononi mwa polisi, Ndio Mzee, Chemsha Bongo, Good Boy, Show Love, Niaje ni Vipi, Alikufa kwa Ngoma nakadhalika. Kwakweli hamna jambo la kijamii ambalo hiphop haijaligusa, kuna maktaba ya kutosha itakayosomwa vizazi na vizazi kwa maAna muziki haufi.

Lakini katika upande wa kuwa fursa ya kuwatoa vijana bado haijafanya kazi kubwa kwanini?

Haswa kipindi hiki ambacho biashara ya muziki inakuwa kubwa Afrika na bila shaka afro beat ndio muziki namba moja Afrika.Kuna mawazo miongoni mwa wana hiphop ambayo yanachanganya na kupoteza mwelekeo wake, kwa ambao hawata yatafakari.

Mawazo hayo ni kuwa hiphop ndio muziki wa kitaa lakini, ukiwa kitaani, bodaboda, bajaji,saloon,klabu, masherehe kadhalika unaskia sana muziki ya kuimba moto, Vanessa,Barnaba, chache za rap. Sasa hicho kitaa tunachomanisha ni kipi? Wakuimba wao hawaishi kwa imani wanapushi muziki yao kote kwenye harusi,mabaa,mageto, magari, vipindi vya asubuhi mpaka usiku kote wamo.

Hip hop sio muziki wa media, lakini ndio wanaongoza kuwashambulia na kuwalalamikia watu wa media na kuwatukana kwenye nyimbo? Kivipi sasa na hiphop sio muziki wa media? Wakuimba wako bize kutafuta connection za media ndani na nje ya nchi.

Sisi ni hiphop wale sio, wale laini hawakazi, commercial lakini! Hip hop si ni uhalisia wa mawazo ya mhusika, experience yake ya maisha aliyopitia, sasa unawezaje kujudge experience ya mtu na ukasema sio ya kweli(not real) wakati wewe haujaipitia. Ni upotezaji focus, lini umeskia afro beat wanasema sisi ndio wale sio?

Ushindani wa kushambuliana utaskia, madogo wameteka gemu wakongwe wanahanya. Wakuimba wanashindana videos, colabo za kimataifa, mavazi nakadhalika vitu vinavyoongeza thamani ya muziki.

Hip hop sio muziki wa biashara kweli? 2pac kauza kopi zaidi ya milioni 75, movies, mavazi kama rocawear, G-unit, labale kubwa kama Rock nation vyote hivyo vimefanyika kupitia hip hop. Jay Z, ana zaidi ya dolla milioni 800, Dre sasa ni billionaire. Waimbaji wanaongea biashara na kujaribu vitu vikubwa, hip hop ina fursa kubwa lakini haya mawazo yatakwamisha wengi.

Waimbaji wana bifu zisizo na madhara wanagombania mara wasichana ama mambo ya kiki na zinawapa media platform na kuwakuza, hiphop matusi tena mabaya, kutishiana mpaka kushambuliana na kuumizana, nakadhalika, ni kuiangusha!

Anapotokea mwana hip hop anayetaka kujaribu muziki wake kufikia watu wengi na kuwa na matumizi mengi yaani club, ghetto, kwenye mabar, vipindi vyote, harusi, watu wa kwanza kumvuta shati watakuwa wana hiphop! Utaskia ‘hakazi tena yule, ile laini’ badala ya kumwona kama mtu anayetanua wigo,soko na kuongeza fan base na kufanya watu wengi kuwa karibu na hip-hop

Kuzuia ubunifu wa kistyle, biti, melodi, ushairi. Katika hii dunia inayokwenda kwa speed kali angalia matoleo ya simu yote ni kupata wateja wengi, kuboresha huduma na kufanya isichoshe watumiaji. Angalia afro beat wanavyobadili. Akina Wizkid, P-Square, Diamond, leo wamepiga dansi hii kesho hii, mpaka wanaruka na parachute kwa video. Hip hop kivipi ibaki vilevile? Generation zinabadilika, dunia inabadilika J-Cole hawezi kuwa Nas wala 2 Pac.

Je kusipokuwa na mifano ya wana hip hop waliofanikiwa, mzazi gani ataruhusu mwanae afanye hip hop na huo si ndio mwanzo wa kukosa vipaji vipya!

Makala hii nimeandika kwaajili ya wadogo zangu wenye kipaji huko form one. Msiwe kama sisi kuweni tofauti. Harakati ni pana Staki Kazi itakwambia ujiajiri, Diamond, Joh Makini, Vanessa watakuonesha kwa vitendo namna ya kujiajiri na wote hapo ni wana harakati kwa kuonesha jamii njia.

Mfuate Nick wa Pili kwenye Twitter na Instagram kwa jina >> @nikkwapili

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents