Bongo Movie

Kiingereza siyo tatizo – Irene

Irene“Kiingereza hakikuwa tatizo kwangu kwani nimeanza kuongea lugha hiyo tangu nikiwa mtoto mdogo iweje leo nionekane sijui wakati hata kwenye shindano la kumtafuta mrembo wa Temeke niliongea kiingereza?.

Irene“Kiingereza hakikuwa tatizo kwangu kwani nimeanza kuongea lugha hiyo tangu nikiwa mtoto mdogo iweje leo nionekane sijui wakati hata kwenye shindano la kumtafuta mrembo wa Temeke niliongea kiingereza?.

“Sikukaririshwa swali na wala sio kwamba sijui kiingereza nafahamu sana ila sijui kilichotokea pale”.

Hayo ni maneno ya Irene Uwoya ambaye alishika nafasi ya tano katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mrembo wa Tanzania katika mashindano yaliyofanyika Agosti 5 ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuondoka na kitita cha fedha taslimu shilingi milioni moja na nusu, aliyoyasema katika ofisi za Bongo5 muda mfupi kabla ya kupaa kuelekea nchini India kwa ajili ya kusomea kozi ya Computer Science.

Irene Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Miss Temeke alisema,

“Nilikuwa na matumanini makubwa ya kufanya vizuri, sikutegemea kuwa nje ya Top 3.

“Nashindwa kuelewa ni kitu gani kilichonifanya nishindwe kujibu swali na kushikwa na kigugumizi nikiwa jukwaani vinginevyo ningeibuka na moja ya nafasi za juu zaidi”-Irene.

Mrembo huyu baada ya kushindwa kujibu swali alirudi back stage na kuanza kujisikia kizunguzungu ambacho kilimpelekea kuanguka na kupoteza fahamu.

Pamoja na yote Irene ameyakubali matokeo kwani anasema tangu wako kambini wengi wa mamiss wenzake walitegemea kuwa mrembo Jokate Mwangale ambaye alishika nafasi ya pili ndiye atakayekuwa Miss Tanzania , kitu ambacho hakikutokea na taji la Vodacom Miss Tanzania 2006 kutua kwa Wema Sepetu.

Irene Uwoya amebainisha kuwa mbali na masuala ya urembo pia ni mwanamuziki na tayari ameshaandaa wimbo tayari kuingia studio na kuchomoka na single yake ya kwanza.

 

Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents