Promotion

Leo ni Leo Katika MAMAs

diamond_lagos

Ni kiasi cha miezi 3 tangu tuzo za Muziki MAMAs 2010 zinazoandaliwa na kituo chako cha televisheni MTV Base kuzinduliwa rasmi jijini Lagos ambako sherehe za tuzo hizo zinafanyika.

 

Leo ndio siku ambayo wasanii mbali mbali toka bara la Afrika na wachache kutoka ulaya pamoja na bara la Amerika watatuzwa kwa kazi zao ambazo zimepigiwa kura na wadau wapenzi na mashabiki wa muziki wa kiafrika ambao kwa miezi mitatu wamekuwa wakijinadi kwao.

Tayari maandalizi yote yanayohusiana na sherehe hizo za tuzo kwa wasanii wa Ki Afrika ambazo zinafanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 yamekamilika.

Wasanii wote kuanzia watakaotoa burudani, waburudishaji na wawania tuzo wamewasili jijini Lagos na wako tayari kubeba tuzo ambazo zitafanyika katika ukumbi wa Eko Expo Center katika hoteli ya EKO SUITES iliyopo ndani ya mji wa Victoria Island katika wilaya ya Ikoyi jijini Lagos.

Msanii Diamond ndiye pekee anayebeba bendera ya Tanzania katika tuzo hizo za MaMas na jana alasiri wakati akiongea na mwakilishi wa bongo5 aliwataka watanzania kuendelea kumpigia kura bila kuchoka ili kumpa nafasi ya kubeba tuzo.

Bongo5 itakuletea habari kamili ya sherehe nzima inayotarajiwa kuanza majira ya saa kumi na moja na nusu jioni kwa wageni mbali mbali waalikwa kuwasili kabla ya sherehe za tuzo hizo kuanza rasmi majira ya saa 3 kamili usiku kwa saa za hapa Lagos ambako kwa Tanzania itakuwa saa moja usiku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents