Siasa

Machinga Complex Haliko Sawa

JENGO jipya kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga, linaloendelea kujengwa jijini Dar es salaam, si salama kwa binadamu kwa kuwa baadhi ya vipimo havikuzingatia matumizi ya jengo.

JENGO jipya kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama machinga, linaloendelea kujengwa jijini Dar es salaam, si salama kwa binadamu kwa kuwa baadhi ya vipimo havikuzingatia matumizi ya jengo.

Hayo yamebainishwa jana na timu ya bodi ya wasanifu na wakadiriaji majengo iliyotembelea jengo hilo lililopo katika makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kulikaguzi jengo hilo linalotazama Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, msajili wa bodi hiyo, Abraham Marres alisema ngazi za kupandia kwenda juu za jengo hilo ni ndogo za kuwezesha watu wawili tu kupita kwa wakati mmoja hivyo kuwa hatari wakati kunapotokea matatizo yanayotaka watu wengi watoke kwa wakati mmoja.

Alisema hali hiyo ni tofauti na kimo cha maghorofa ya jengo hilo, ambalo lilitembelewa na Rais Jakaya Kikwete miezi michache iliyopita.

“Hapa hebu tuweke pembeni siasa, hizi ngazi ni nyembamba haziwezi kufikia upana wa zile za soko la Kariakoo ambalo limejengwa muda mrefu uliopita wakati mahitaji pamoja na idadi ya watu sio kama hii ya leo,” alisema Marres.

Aliongeza kuwa, japokuwa hakuwa amepewa michoro ya jengo hilo ili kuweza kufanya ulinganifu kutokana na wahusika kutokuwepo kwenye eneo la ujenzi, bado uwazi kati ya paa na urefu wa mtu (headroom) katika kila ghorofa ni kidogo ukilinganisha na msongamano wa watu watakaoingia katika jengo hilo.

Ukaguzi wa jengo hilo umefanyika kutokana na bodi hiyo kuamua kupitia majengo makubwa yanayoyojengwa jijini Dar es Salaam ili kujionea kama sheria za ujenzi zinafuatwa na wataalamu wa fani hiyo.

Bodi hiyo jana ilifanya ukaguzi wa majengo mawili- Machinga Complex na jengo la ghorofa kwa ajili ya nyumba za polisi linalojengwa kando ya Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ukaguzi huo, mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Ambwene Mwakyusa alisema imefikia wakati kwa wajenzi wote kutumia wataalam wa majengo ili kuondokana na adha ya kuanguka mara kwa mara kwa majengo hapa nchini ili kurejesha heshma ya taaluma hiyo ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi (Architect and Quantity surveyor).

Aliongeza kuwa kama taratibu hizo zitakuwa zinafuatwa basi itakuwa rahisi kuwawajibisha wabunifu majengo ambao katika taratibu za majenzi wao ndio huwa wanatakiwa kuwa wasimamizi wakuu wa ujenzi unaokuwa unaendelea

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents