Bongo5 Makala

Makala: Watu 7 maarufu waliozungumza kuhusu Diamond na Alikiba

Kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli, unapotaka kuzungumzia muziki wa wa Bongo Flava ni vigumu kuepuka kutaja la Diamond Platnumz na Alikiba.

Muziki wao, ushindani na maneno ya hapa na pale yanatoa picha halisi ya game ya muziki huo ilivyo kwa sasa. Kutokana na uzito wa majina yao na kile kinachoripotiwa kuwa hawapatani (beef) si ajabau kusiki watu maarufu wakiwazungumzia. Makala haya fupi yanakuletea watu maarufu waliozungumza chochote kuhusu wawili hawa.

  1. AmaniĀ 

Msanii huyo kutoka nchini Kenya katika mahojiano yake na kituo cha Radio Citizen March 2016, alizungumzia jinsi Diamond na Alikiba anavyolipwa fedha nyingi pindi wanapoenda kufanya show katika nchi hiyo kitu ambacho alisema si kibaya.

Ni kitu ambacho kipo kila mahali, hata ukienda kuperform Rwanda atakuta wewe unalipwa hela nyingi zaidi vile wanalipwa, lakini pia wasanii wajitahidi ili waweze kushindana katika jukwa la Afrika Mashariki na Afrika at least wawe na kitu kinaitwa bargain power.

Nyimbo zako zikiwa ni hit zina video ambazo ni kali uko na bargain power na unaweza itisha kiasi cha juu zaidi kwa hiyo ni hali ya biashara hamna haja ya kuumia.

Kuna watu ambao sio lazima wawe na hit lakini huyo mtu akishika hiyo stage anaperform quality show na utakuta hao watu huperform kwenye hizi event za mabalozi hulipwa fedha nyingi sana.

2. Ruge Mutahaba

Ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, November 2016 kupitia XXL alizungumzia team ambazo kazi yake ni kuwashabikia Diamond na Alikiba na kueleza namna wasanii hawa wanavyoweza kunufaika kwenye hilo na mathara yake.

Ishu ya team zilikuwepo na haziitakaa kuacha kuwepo, tatizo la team ni kwenye athari za wale wanateam, yaani mimi naamini team ni muhimu kwa sababu zinaleta ushindani lakini team ya kumshangilia kwenye mitandao kwangu sioni kama ni team ya ukweli.

Team ni kusapoti mpaka mwisho, team ni akifanya tamasha wale wa team nusu yao wamo ndani, ndio tuzungumze team kwa maana hiyo na hizo ndizo zilikuwa team Simba, Yanga, Liverpool, Manchester, team inamnunua mchezaji inarudisha hela siku hiyo hiyo kwa jezi kununuliwa na watu wale wa ndani ya hiyo team.

Lakini hii team ya kushabiki juu kwa juu kweli kwangu haina athari sana kama haitaleta athari ya kibiashara inabakia ni ushabiki tu wa kawaida.

Inaweza kuleta matatizo, matatizo ya Tupac na B.I.G sikulikuwa na team, Tupac alipigwa siasi na watu wa B.I.G, tuombe Mungu yasitokee matitzo hayo. Kwa bahati mbaya huwezi kulazimisha kwa kutokuwepo kwa team kwa sababu wapo wanaopenda Msondo na wanaopenda Sikinde, suala ni kwamba unasaidiaje kile unachokipenda kiwe na maana na kizidi kukua.

3. Salim Kikeke

Mtangazaji huyo wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, September 2015 katika kipindi cha Mkasi kilichokuwa kikiruka EATV aliulizwa kati ya Alikba na Diamond anafikiri nani mbabe zaidi.

Nisingependa kuchukua upande mimi naheshimu kazi zao na wote nimefanya nao kazi, Alikiba sijawahi kufanya nae interview lakini nakumbuka tulishapanga tukakubaliana kabisa tufanye lakini akapata safari. Diamond alipokuja Uingereza nikamwanbia ukiwa na nafasi njoo kwenye kipindi chetu akakubali na akaja tukafanya nae interview.

Kwa mtazamo wangu mimi kama mwandishi wa habari ambaye pia napenda kukuza muziki wetu wa Tanzania nasema sichukui upande wowote naheshimu kazi zao.

4. Vera Sidika

Huyo ni video vixen kutoka nchini Kenya, August 2016 katika mahojiano na Bongo5 aliulizwa kati ya Diamond na Alikiba anamkubali nani zaidi.

Mimi namsikiliza Diamond, muziki wake na stayle yake ni tofauti kisha nzuri pia namuona anarelease hit after hit, hatulii yeye hutia bidii kila siku halafu si muziki pekee yake pia anaweza kusaidia vijana na kuwapatia nafasi ya kukuza vipaji vyao kama sasa hivi kuna artists wapo chini yake which is good thing.

Mtu ukiwa katika industry especially music it good to empower the people maana yake kuna watu wengi wanakuangalia wewe na wana kipaji lakini hawajui waende vipi sasa wewe ukiwaonyesha direction inakuwa ni vizuri sana.

5. Dkt. Harrison Mwakyembe

Kwa sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, March mwaka huu baada ya kupata taarifa ya kuwa Diamond na Alikiba wameshindwa kurekodi wimbo kwa ajili kuhamasisha watu kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys alisema atahakikisha wanapatana.

Hao vijana niwaite hapa Dodoma na sitaki kusikia wengine wanasema unajua wale hawakai pamoja, hamna lolote mimi baba yao watakaa pamoja, hapa tupo kwenye mambo ya taifa, hili ni suala la kitaifa lazima tulifanikishe na kila mtu achangie.

6. Dudu Baya

Msanii huyo wa Bongo Flava July 2014 kupitia Amlifaya ya Clouds Fm aliwataka Diamond na Alikiba kutambua wao ni wakina nani na wana uwezo wa kufanya nini, pia watumie fan base walionayo kujinufaisha kibiashara kuliko kusikiliza maneno ya watu ambayo yamelenga kubomoa.

Alikiba alifanya ngoma na R Kelly mimi nilifurahia sana nilipenda kinoma na nikapiga saluti kwa kuwa mdogo wangu kwamba anaenda next level, Diamond kaja kufanya vizuri nina appreciate.

Muziki unakosa power kwa sababu ya watu kuwa na roho mbaya na chuki na kutokuwa makini na watu waliotuzunguka, kuna mtu anaenda kwa Alikiba anasema hivi, anaenda kwa Diamond anasema hivi.

Kwa hiyo hawa kama wadogo zangu mimi nawashauri watulie chini wajitambue wao ni wasanii na usanii wao ni wa kutengeneza pesa, tena hata watengeneze tour ya amani wazunguke nchi nzima watengeneze hela na si beef.

7. Kingwendu

Mchekeshaji huyo January 2016 aliiambia Bongo5 kuwa yeye akipata airtime katika radio na tv kama wanavyopata diamond na Alikiba atafika mbali kimuziki.

Mwaka jana nimetoa nyimbo tatu lakini zote hazikupata airtime ndio maana hazikufanya vizuri lakini kwa sababu ni nyimbo nzuri zingepata airtime ningeshindana na akina Ali Kiba na Diamond ambao wanafanya vizuri.

Sijakata kataa, mwaka huu kuna kazi mpya nimeziandaa pamoja na video mpya. Pia nikifanikiwa kupata meneja wa kusimamia muziki wangu natumaini nitafika mbali sana kwa sababu muziki wa sasa ni mipango tofauti na ule wakati nimetoa Mapepe.

Nimejaribu kugusa kila kona ambayo kwa namna moja au nyingine inahusika katika muziki wa Bongo Flava ili kujionea nguvu ya ushawishi walionayo Diamond na Alikiba. Kufikia hapa sina budi kuweka kalamu yangu chini, asante sana.

By Peter Akaro

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents