Siasa

Marekani haijui aliko Balali

SERIKALI ya Marekani haijui aliko Gavana wa zamani wa Benki Kuu (BoT), Dkt. Daudi Balali na haina sababu ya kumfuatilia.

Na Mwandishi Wa Majira

 

SERIKALI ya Marekani haijui aliko Gavana wa zamani wa Benki Kuu (BoT), Dkt. Daudi Balali na haina sababu ya kumfuatilia.

 

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green, alisema nchi yake haiwezi kumfuatilia mtu kwa kuwa ni kuingilia uhuru binafsi.

 

Alisema anachojua ni kuwa Serikali yake ilimnyang’anya viza ya nchi hiyo, baada ya Serikali ya Tanzania kumwondoa katika wadhifa wake wa ugavana.

 

“Huyu alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini Marekani na viza yake ilikuwa ya hadhi hiyo, hivyo kutokana na hatua ya nchi yake nasi tuliamua kumnyang’anya viza yetu,” alisema Balozi Mark.

 

Hata hivyo alisema ni jukumu la Serikali ya Tanzania kumfuatilia raia wake kokote aliko duniani.

 

Balozi Green alisema Serikali yake huwa makini zaidi katika kuangalia nani anayeingia nchini humo na si anayeondoka, lakini akasisitiza kuwa Dkt. Balali bado hajafukuzwa nchini humo.

 

Balozi Green aliitisha mkutano na wahariri hao kuwaeleza rasmi ujio wa Rais George Bush wa Marekani, baadaye mwezi ujao ambapo pamoja na kukutana na viongozi wa nchii ataangalia maendeleo ya miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikifadhiliwa na nchi yake.

 

Rais Bush anatarajiwa kufanya ziara ya nchi tano za Afrika kuanzia Februari 15 hadi 21 mwaka huu, ambapo pamoja na Tanzania atafika Benini, Rwanda, Ghana na Liberia.

 

Balozi Green alisema akiwa katika ziara hiyo, Rais Bush atajadili na viongozi wa mataifa hayo, jinsi Marekani inavyoweza kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika katika ujenzi wa demokrasia, heshima za haki za binadamu, biashara huria, uwekezaji na kuwa na fursa zaidi za biashara.

 

Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents