Michezo

Mbivu na mbichi kujulikana leo urais TFF Dodoma (Picha)

Wajumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hii leo Agosti 12 wanapiga kura mkoani Dodoma kuchagua viongozi wapya watakao simamia mchezo wa soka hapa nchini.

Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya TFF, Steven Mashishanga (kulia) na Joel Bendera (katikati) wakiwa pamoja na katibu mkuu wa baraza la michezo, Mohammed Kiganja (kushoto)

Jumla ya w agombea 65 wapo Dodoma tangu Jumatano wakitengeneza mazingira kwa wapiga kura huku kila mgombea akionekana anapambana kivyake kuomba kura na ulinzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ukiwa umeimarisha kila kona jambo ambalo linawapa hofu wagombea kufanya mambo tofauti na kanuni, taratibu na sheria za nchi.

Hapo jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi  wa (TFF), Wakili Revocatus Kuuli aliwaambia wagombea kuwa, wapo huru kufanya kampeni zao hadi asubuhi ya leo Jumamosi kabla ya upigaji kura kuanza.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwasili nje ya ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar mjini Dodoma ambako mkutano mkuu wa TFF utafanyika sambamba na uchaguzi wa shirikisho hilo, amewataka wajumbe wote 128 watambue kuwa watanzania wanawategemea katika kuhakikisha wanawachagulia viongozi bora watakaolisaidia sola Tanzania kusonga mbele

Wakati huo huo TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) imewatahadharisha wagombea na wapiga kura kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu wa TFF na kwamba kiongozi atakayeingia madarakani akibainika kuingia kwa njia ya rushwa wataondolewa madarakani.

Mpaka sasa wadau na wapenzi wa mpira wa miguu nchini wanashauku kubwa ya kutaka kumpata kiongozi atakaye weza kulivusha soka la Tanzania kutoka hapa lilipo na kulifika mbali.

Picha zikiwaonyesha wajumbe na wagombea wa mkutano mkuu wa TFF wakiwasili wakiwasili katika ukumbi wa mikutano wa St. Gaspar mjini Dodoma


Tenga akiwasili akiwa na J. Bendera

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents