Habari

Mbunge ataka twende ZNZ kwa Passport

Mbunge wa Jimbo la Konde Visiwani Zanzibar, Mohammed Said Issa ameishauri Serikali kurejesha utaratibu wa kutumia hati ya kusafiria (Passport) kuingia visiwani Zanzibar ikiwemo Wananchi wanaotokea Tanzania Bara ili kuvilinda visiwa vya Zanzibar kwa kudhibiti Watu kujaa Zanzibar hadi kuhatarisha Watu kukosa sehemu za kuishi.

Mbunge Issa ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambapo amesema Zanzibar ina eneo dogo hivyo ni lazima lilindwe.

“Sikubaliani na suala la kutovilinda Visiwa sasa hivi Zanzibar imekuwa imejaa Watu na tunavyoendelea sasa Zanzibar Watu watakosa sehemu ya kuishi, nampongeza Karume kwa kujenga yale majengo makubwa kwasababu alitaka Watu wote wakae mule kwasababu Zanzibar ni ndogo sana kwa hivyo Mimi bado nahitaji passport irudi ili kuwe na ulindaji wa Wananchi kuingia Zanzibar”

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

CC:Millard Ayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents