Michezo

Messi apiga ‘hat-trick’, Suarez aibeba Uruguay

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi usiku wa jana amefunga mabao matatu ‘hat-trick’ dhidi ya Ecuador nahivyo kuiwezesha timu yake kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi.

Katika mchezo huo Argentina wametoka nyuma wakiwa ugenini na kupata ushindi wa mabao 3-1 huku nyota huyo Messi akifunga mabao hayo na kujihakikishia kufuzu kombe la dunia.

Argentina sasa inaungana na Brazili,Uruguay na Colombia kuelekea nchini Urusi hapo mwakani.

Luis Suarez ametupia mara mbili wakati timu yake ya Uruguay ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bolivia na hivyo kukata tike ya kufuzu huku suluhu waliyo ipata timu ya taifa ya Colombia ya mabao 1-1 dhidi ya Peru imewafanya nao kuwa miongoni mwa timu hizo zitakazo shuhudiwa huko Urusi.

Peru iliyomaliza nafasi ya tano huko Amerika Kusini italazimika kusubiri mchezo wa ‘play-off’ dhidi ya  New Zealand wakati mchezaji wa klabu ya Arsenal,  Alexis Sanchez hatutamuona katika michuano hiyo baada ya timu yake ya taifa ya Chile kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Brazili.

Kikosi cha  Ecuador: Banguera (6), Velasco (6), Renato Ibarra (7), Romario Ibarra (6), Jose Cevallos (6), Ordonez (6), Arboleda (6), Ramirez (6), Intraigo (6), Orejuela (6), Aimar (6)

Waliyokuwa benchi: Uchuariat (6), Valencia (6), Estradaat (6)

Kikosi cha Argentina: Romero (6), Mercado (6), Mascheraho (6) , Otamendi (7), Salvio (6), Perez (6), Biglia (6), Acuna (6), Messi (10), Di María (8), Benedetto (6).

Waliyokuwa benchi: Icardi (6), Fazio (6)
Lionel Messi amekuwa mchezaji bora wa mchezo huo
‘Man of the match’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents