Michezo

Mesut Ozil akataa ofa ya kupokea pauni mil. 1 kwa wiki, wakala wake aadai hayo ni mapenzi yake kwa Arsenal

Nyota wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil amekataa ofa yakuwa anapokea mamilioni ya fedha kwa wiki ambayo yangemuwezesha kuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi duniani hii ni kwa mujibu wa wakala wake, Dr Erkut Sogut.

Ozil ambaye ni raia wa Ujerumani alikuwa amesaliwa na muda mchache wa kuwepo Arsenal kutokana na mkataba wake kuelekea ukingoni kabla ya kuingia kandarasi mpya ya miaka mitatu na nusu mwezi Februari iliyomfanya aweanachukuchua kiasi cha pauni 350,000 kwa wiki na hivyo kumuwezesha kuwa mchezaji anayevuta fedha ndefu zaidi kuliko wote ndani ya timu hiyo.

Kupitia mahojiano yake na Evening Standard, Sogut amesema kuwa Ozil alikataa ofa kutoka ‘Asia’ ambayo ingemfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza duniani kulipwa pauni milioni moja kwa wiki.

”Tulipata baadhi ya ofa kubwa kutoka Asia, kweli zilikuwa ofa zaajabu sana lakini fedha siyo kitu kikubwa sana kwa Mesut,” amesema Sogut ambaye ni wakala wa Ozil.

”Nikweli fedha ni kitu muhimu kukifikiria lakini watu lazima wakumbuke kuwa uwezo wa soka ni moja kati ya vitu vinavyopaswa kuwa na makubaliano.”

”Hii imekuja kutoka tu ndani ya moyo wake, tulikuwa huru kusaini klabu nyingine lakini mwishowe, Mesut aliipenda Arsenal. Maamuzi yote nilimuwachia mwenyewe na mwisho akasema hapa ni nyumbani kwangu nahitaji kuendelea kuwa hapa.”

Ozil ametuwa Arsenal akitokea kwa miamba ya soka ya Hispania na mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya timu ya Real Madrid mwaka 2013.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents