Technology

Miaka 45 ijayo nusu ya ajira duniani zitachukuliwa na roboti, Wataanza kuandika vitabu, kufanya upasuaji na kuendesha malori

Roboti ni kifaa cha kielektroniki chenye uwezo wa kimakenika, kinachotumika kufanya yaliyo nje ya uwezo wa binadamu. Japo kifasihi roboti ni sawa na mtumwa.

Asili ya jina roboti ni lugha ya Kicheki yenye maana ya “mfanyakazi”. Mnamo mwaka 1920 Mwandishi wa vitabu, Josef Čapek aliandika tamthilia inayosimulia hadithi za viumbe wanaotengenezwa kama wafanyakazi na kutumia jina la “labori” kwa lugha Kilatini, lakini baadae kaka yake alimshauri kutumia neno lenye maana hiyo hiyo ya Kicheki ikawa “Roboti”.

Roboti hutumia mitambo na programu maalumu kuiongoza. Roboti za siku hizi zinauwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea. Hazihitaji tena uongozwaji wa moja kwa moja mfano kwa kubonyeza kitufe au kutumia sauti.

Roboti yawezakuwa imeundwa aidha kwa chuma au mwili wa kawaida. Na baadaye kuwekewa akili bandia (Artificial Intelligence). Wengi tumezoea kuona zile za chuma kwenye filamu. Na hatujazoea kuona zenye muundo kama wa binadamu.

Kuna aina kuu 6 za Roboti nazo ni Roboti Sahili, Roboti za Usalama, Roboti za kutoa huduma, Roboti za Viwandani, Roboti Vichezeo na Roboti za kijeshi.

Roboti zinafanya kazi lukuki duniani. Na kila siku zinazidi kuongezeka, Zikifanya kazi kama uhudumu hotelini, viwandani na hata safari za nje ya dunia. Kwa mujibu wa Jukwaa la @worldeconomicforum miaka 10-35 ijayo roboti zitakuwa ni sehemu ya maisha yetu.

Roboti hutengenezwa ili kufanya kazi moja tu, ila kwa ufanisi wa hali ya juu. Roboti hutegemea vifaa viitwavyo microprocessor. Ili kutimiza kazi yake. Kifaa hiki ndio hutumika kama ubongo kwa roboti. Kifaa hicho (microprocessor) ndicho hutoa majibu roboti ifanye nini, kulingana na mazingira yake.

Je, Roboti wanaweza kuchukua nafasi ya mwanadamu kwenye ajira?

Kwa mujibu wa jukwaa la World Economic Forums imeelezwa kuwa miaka 45 ijayo kazi nyingi zinazofanywa na binadamu kwa sasa zitafanya na roboti kwa asilimia 50%, Huku wakieleza kuwa hadi kufikia miaka 120 ijayo kazi zote zinazofanywa na binadamu isipokuwa wanasaikolojia zitafanywa na roboti.

WEF wamesema kuwa 2024 roboti watakuwa na uwezo wa kutafsiri lugha mbalimbali, Na hadi kufikia 2026 watakuwa na uwezo wa kuandika insha (essay).

2027 Roboti watakuwa na uwezo wa kuendesha malori, 2031 watakuwa na uwezo wa kuuza maduka ya jumla na rejareja.

Mpaka kufikia mwaka 2049, Roboti watakuwa na uwezo wa kuandika vitabu, 2053 Roboti watakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji mdogo kwa binadamu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents